Fikra za dijito: 20k yangu ya kwanza kama Social media influencer.

“Good Afternoon, My name is ………………. . I work as an analyst at …………. . We are working with various clients in the developmental sector. Your profile is very thematic .We are looking to begin a micro influencer fellowship will you be interested to join? What will you be your monthly estimate? “. Huu ni ujumbe nilioupokea June 21, 2021, ikiwa ni almost mwaka mmoja baada ya kuwa serious an mitandao ya kijamii.

Sikuwa nafahamu chochote kuhusu social media influencing na wala sikuwa nafahamu kama kurasa zangu za mitandao ya kijamii ninazotumia kupoteza muda na kuenjoy kwamba kuna kipindi zinaweza kuniingizia kipato. Nilitazama ujumbe ule mara mbili mbili bila kuwa na majibu ya moja kwa moja kwa aliyenitumia ujumbe ule, akisoma makala hii najua natacheka sana.

Baada ya kupokea ujumbe huu ilibidi niwaone wataalamu wa kazi hizi {Watu waliofanya kazi hizi kwa kipindi kirefu}, Kuwapata haikuwa ngumu though changamoto kubwa ilikuwa kupata majibu niliyotarajia kutoka kwao. Nikisema nisimulie simulizi hii ninaimani tunaweza kaa siku nzima hapa na tusiimalize, ila kwa sasa embu kamata kinywaji chako kisha shuka taratibu na andiko hili

Social Media influencing ni nini?

Kila mtu ana namna yake anayotafsiri social influencing huku wengi wetu tukihusisha na mtu kuwa na followers wengi.Mimi sikubaliani nanyi wakuu wala siwapingi pia maboss wangu, ila kwa utaalamu wangu mdogo ngoja niwape tafsiri yangu ndogo kuhusu social media Influencing.

Neno social media influencing msingi wake ni neno “Influence” ambao kimsingi maana yake ni nguvu ya kushawishi watu kufanya jambo fulani ambapo mara nyingi nguvu hii inatokana na authority aliyo nayo mtu, mahusiano yake na hadhira yake pamoja na maarifa aliyo nayo mtu husika.

Kwa minajili hii tunaweza sema Social media influencin ni nguvu ama uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii kushawishi watu kuchukua hatua fulani.

Social Media influencer wa Tanzania wanaingiza kiasi gani?

Hili nilitaka niliweke mwisho kabisa, ila nikasema wala ngoja niiweke mapema kabisa ili wazee wa maokoto waamue kama wanamaliza kusoma andiko hili la dijito hadi mwisho ama waishie hapa.

Binafsi sijui kiasi ambacho social media influencer wengine wanalipwa kwa kampeni, japo ninaona ona kama nyie kuhusu 20k. Influencer kabla hajalipwa kiasi chochote huwa anapimwa kwa vitu vifuatavyo

  • Idadi ya wafuasi alio nao na hapa ndipo huwa wanagawanywa kwenye makundi kama mshawahi skiaga Mega, Macro, Nano na Micro

  • Aina ya maudhui wanayo chapisha na hapa ndio vitu kama Blogs, podcast na social media posts ndio zinaangaliwa

  • Ukubwa wa ushawishi wako na hapa huwa tunagawanywa kwenye makundi mawili watu mashuhuri ie wasanii, machawa nk na kundi jingine wanaitwa opinion leaders nan hapo ndipo tunakaa watu kama sisi tuliojichimbia kwenye niche zetu

Kimoyo moyo mshaanza kusema mbona dijito hataji analipwaga kiasi gani, tutafika tulieni ndugu zangu. Kwenye hizi kazi mimi nawajua wadau muhimu watatu ambao nimefanya nao kazi hadi sasa ambao ni pamoja na majukwaa ya kutoa kazi kwa influencers, agency za masuala ya masoko na makampuni yenyewe.

Kikaangoni: Majukwaa ya kutoa kazi za influencing zimekulipa kiasi gani bwana dijito?

Asante kwa swali zuri sana ndugu mwandishi, Binafsi sina experience nzuri na majukwaa haya na kwa kuzingatia hilo sitoyataja kuepusha vurugumai za hapa na pale. Mara nyingi majukwaa haya huwa wanachukua kazi kwenye makampuni moja kwa moja na kulipa influencers. Kampuni hizi nyingi bado zina changamoto hususani kwenye mifumo yao ya malipo na namna yanachagua influencers.

Kampeni nyingi kwenye majukwaa haya huwa zimelenga kuongeza uelewa kuhusu bidhaa husika kwa watumiaji zaidi na ndio maana mara nyingi huwa zinajikita kuwa na influencer wengi kuliko kuwa na quality influencer.Maudhui mengi kwenye majukwaa haya huwa static na wewe kazi yako ni kubandika maudhui husika kwenye kurasa yako ya kijamii.

Binafsi mara nyingi huwa naepuka kupokea deals zao kwani malipo yao huwa kiduchu mara nyingi aina ya kazi zinazowekwa huko huwa haziendani na hadhira niko nayo.

Tangu nimeanza kufanya na majukwaa haya huwa yananilipa Tsh 10k hadi 15k kwa post moja

Kikaangoni 2: Dijito tuambie agency za masoko zimekulipa kiasi gani?

Mwandishi japo umenibana sana na hutaki nitafute pa kuchoropokea hivyo sina budi kusema kweli kama Dula Makabila.Agency za marketing ni moja ya watu wenye dili nyingi sana za influencing kwenye nchi hii ya mama kizimkazi. Kampuni nyingi zinachagua kufanya kazi kukwepa stress zinazokuja kwenye kufanya kazi na influencer moja kwa moja.

Agancy za masoko huwa wajanja wajanja sana kwenye kulipa influencer na wanawajulia kweli kweli. Kwenye kampeni zao mara nyingi huwa kila influencer huwa ana hela zake. Uzuri wao wanakuuliza rate card zako kabisa sasa kazi kwako kuweka rate cards za kueleweka ama la.

Binafsi nina bahati ya kufanya kazi na agency za local na global. Napenda sana kufanya kazi na agency za kimataifa kuliko za nyumbani. Agency za nyumbani mara nyingi huwa haziko straight forward huku agency za wenzetu huwaga wakogo moja kwa moja

Kampeni zote nimefanya na agency za local bugted zao huwa wanaanzia Tsh 150k huku zile za Global wakianzia na Usd 300.

Kikaangoni 3: Makampuni yanakulipa kiasi gani kwenye gig za Influencing?

Binafsi napenda sana kufanya kazi na kampuni moja kwa moja kuliko hata kufanya na makundi hayo mawili ya juu.Changamoto ya kampuni especially za local huwa hawajui wanataka nini ila uzuri wao huwa wanakupa nafasi ufanye unajojiskia cha msingi wao waone matokeo tu.

Binafsi nimefanya kazi na kampuni mbalimbali za kitaifa na kimataifa kwenye kazi hizi za influencing. Kwa kampuni za local vigezo huwa sio vingi sana ila kwa zile za kimataifa huwa zinakuja na maelekezo mengi sana na mara nyingi wanakuwa wameshakufanyia scounting ya kutosha na kuwa na details zako nyingi.

Kampuni za kimataifa ni ngumu sana kukupa gig kama umewahi fanya kazi na competitor wao na huwa wanazingatia sana authenticity ya creator na niching.

Kampuni nyingi za nyumbani malipo yao huwa yanaanzia Tsh 500k na kwa upande wa zile za kimataifa huwa wanaanzia usd 450.

Changamoto ni zipi?

Moja ya eneo lenye changamoto kwenye creative economy ni hili.Changamoto zote zinasababishwa na wadau wote waliopo kwenye eneo hili.Baadhi ya changamoto ni pamoja na

  • Fikra potofu :Watu wengi bado wanaamini influencer ni lazima awe na followers wengi kitu ambacho sio kweli.Kuna brand zinapoteza hela nyingi sana kwa kushindwa kufanya machaguo sahihi za influencer wa kufanya nao kazi.

  • Clients wasio waaminifu:Kimtindo clients inabidi muanze kuheshimu influencers, mtu kakufanyia kazi yako kama ulivyotaka kwanini kwenye malipo tuanze kukimbizana? nimemaliza kazi yako nilipe nanii.

  • Influencers wasio waaminifu :Influencer pia wamekuwa na tabia ya kukimbia hela za clients na kushindwa kutimiza ambacho wameahidi kwa clients. kama unajijua uko na hii tabia mwaka huu 2024 hatukutaki.

Mwidho, haya ni maoni yangu na nimeshare uzoefu wangu tangu nimeanza kufanya hizi kazi, najua huenda kila influencer atakuwa na uzoefu wake wa aina yake huko nje.

Kama unatafuta influencer wa kufanya nae kazi kwenye kampeni tofauti tofauti tafadhali niandikie hapa barakamafole18@gmail.com ama niandikie ujumbe kupitia namba ya whatsapp 0734460217

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *