NILICHOKIZUNGUMZA KWENYE MDAHALO WA TAIFA WA VIJANA – UDOM 2023 {USALAMA MTANDAONI}

Mapema wiki iliyopita nilialikwa jijini Dodoma kuzungumza kwenye mdahalo wa taifa wa vijana. Mdahalo huu uliandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia. Mada kuu ilikuwa kuhusu usalama mtandaoni huku tukiangazia zaidi umuhimu wa kuhakiki taarifa kabla hujachapisha mtandaoni.

Tukio hili lilifanyika kwenye ukumbi wa CIVE uliopo kwenye ndaki ya Informatics, chuo kikuu cha Dodoma. Miongoni mwa makundi ya watu waliohudhuria ni pamoja na viongozi wa kisiasa, viongozi wa taasisi mbalimbali, waandishi wa habari, wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma.

Mgeni rasmi wa tukio hili alikuwa Naibu waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia 

Matukio mengi yalifanyika siku hiyo ikiwemo hotuba za viongozi mbalimbali, burudani tofauti tofauti pamoja na mdahalo wenyewe. Mdahalo uliendeshwa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha serikali, Mr Innocent PM Mungy huku wazungumzaji wenzangu wengine wakiwa 

1. Meshack Kiburwi – University of Dodoma, Student Counsellor

2. Imani Luvanga – Mwanaharakati wa haki za kidijitali

3. Steven Wangwe – Acting director of communication safety and information  technology security 

4.Ngalula Jackson – Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma na peer educator 

Mdahalo ulifunguliwa kwa wasifu mfupi mfupi wa wazungmzaji na kitu kilichonivutia zaidi ni namna mwendesha mdahalo alivyotoa wasifu wangu huku neno ‘kijana mwenye heshima zake’ likisikika zaidi hali iliyoibua makofi kidogo ukumbini. 

Kwenye mdahalo huu nilipata wasaa wa kuzungumza namna ukatili mtandaoni unavyoathiri vijana. Kiasi kikubwa nikizungumzia matendo mbalimbali yasiyofaa yanayoendelea mtandani hususani masuala la Bullying na madhara yake ikiwepo matatizo ya  afya ya akili.

Kama kawaida yangu ajenda ya uchumi wa kidijitali ni suala ambalo popote ninapopata nafasi lazima niligusie, na kwenye mjadala huu nilipata wasaa wa kuiomba serikali iongeze jitihada zaidi kusapoti uchumi wa kidijiti hususani katika kuwaongezea elimu vijana kwenye kufahamu fursa chanya zinazopatikana mtandaoni.

Moja ya kitu nilivutiwa nacho zaidi ni namna ambavyo wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma walivyo wasikivu na makini kufuatilia mjadala huku wakiuliza maswali mbalimbali ya msingi na miongozi mwa maswali waliyouliza ni pamoja na 

1.Kwanini masuala ya ukatili mtandaoni yanawalenga zaidi wanawake na sio makundi mengine?

2.Namna gani wanaweza kutambua tovuti salama na zisizo salama mtandaoni?

3.Ikitokea picha ama video ya utupu ya mtu kuvuja mtandaoni njia gani anaweza tumia kuziondoa?

4.Fursa zipi chanya zinapatikana mtandaoni?

Miongoni mwa maneno niliyasikia mara kwa mara kwenye mdahalo huu ni pamoja na digital footprint, digital permanence, digital identity na digital citizenship.

Mwisho shukrani za pekee ziwaendee National Democratic Institute {NDI} pamoja na Bridge for Change kwa kuwezesha safari yangu hii 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *