Software development itanipa michongo?

power learn hackathon

Kabla sijaandika makala hii ilibidi nipitie maandiko tofauti tofauti kuhusu software development na namna inavyoweza kusaidia watu kujiingizia kipato. Moja ya data iliyonikosha na kunishangaza sana ni kiasi ambacho software developer wanaingiza nchini Tanzania ukilinganisha na kiasi ambacho software developers wa nchi nyingine wanachoingiza.

Kwa mujibu ya tovuti ya Glassdoor wanasema, software developer wa Tanzania wanaingiza kati ya Tsh 1M hadi 5M kwa mwezi. Mbali na Tovuti ya Glassdoor, tovuti ya Mint Salary wanasema hiki ndicho kiasi wanachoingiza software developer wa Tanzania

 • 25% ya software developer wa Tanzania wanaingiza chini ya USD 480
 • 50% ya software developer wa Tanzania wanaingiza USD 540 kushuka chini
 • Asilimia iliyobaki wanaingiza chini ya USD 640

Stadi gani zinatakiwa ili mtu awe mzuri kwenye software development

Hapa kuna aina mbili za stadi ambazo software developer mzuri anatakiwa awe nazo. Stadi hizo ni Hard skill na soft skill, ambapo hard skills mara nyingi ni zile zinazohitaji utaalamu mkubwa wa technical huko softskills ni zile ambazo hazihitaji stadi kubwa za technical

Tuanze na hardskills kwanza

 1. Programming

Programming ni moja ya core skill kwa software developers, ili uwe software developer mzuri hauna budi kujifunza lugha mbalimbali za programming.Kuna programming language mbalimbali ambazo unaweza ukabobea kama software developer hizi ni baadhi

 • Python: Hii inatumika zaidi kwenye masuala ya website development, data analysis, machine learning na automation. Wenyewe wanakwambia python haina utofauti mkubwa na lugha ya kiingereza na watu wengi wanaojua python wanachaguaga kuwa software engineering, data science na wataalamu wa AI.
 • java: Hii mara nyingi inatumika kwenye masuala ya kutengeneza mobile application, kutengeneza Chatbot na program mbalimbali za AI.
 • Kotlin: Hii ni programing language ambayo inaendana na Java kwa kiasi kikubwa. Incase unataka kuwa full stack web developer ni moja ya programming language inayobidi uitupie macho kwa kiasi kikubwa.
 • Swift: Hii ni programming language inayotumiwa zaidi na product za kampuni ya Apple, unaweza tumia hii kutongeneza product kwa ajili ya operating system kama IOS, MACOS na TVOS. Swift unaweza tumia kutengeneza product kwa ajili ya product za Apple kama vile simu, Televisheni, Ipad na Saa.

2. Ufahamu wa namna algorithm zinavyofanya kazi

Namna algorithm zinavyofanya kazi ni moja ya sehemu muhimu kwa software developer kufahamu.Baadhi ya stadi muhimu kwa watu wanaotaka kufahamu namna algorithm zinavyofanya kazi ni pamoja na

 • Hesabu: Wengi tunakimbiana sana hapa, lakini ili uelewe algorithm zinavyofanya kazi kwa undani ni muhimu ujue hesabu mbalimbali kama vile algebra na calculus.
 • Frameworks za machine learning: Framework za machine learning huwa zinatumika kuimplement algorithm mbalimbali, moja ya framework maarufu ni pamoja na tensorflow na pytorch.
 • Programming: Programming nimeizungumzia vizuri sana kwenye point namba moja, moja ya programming language maarufu zaidi kwenye masuala ya algorithm ni pamoja na python na Java

Baadhi ya soft skills kwa software developers ni

 1. Ushirikiano na mawasiliano

Software developer mzuri ni lazima uwe vizuri kwenye kushirikiana na kuwasiliana na wenzako, mara nyingi kama sio zote utajikuta unafanya kazi na wenzako hivyo stadi za kuwasiliana na wenzako ni muhimu. Taratibu taratibu anza kujifunza kutumia tools kama Clickup, Asana, Jira na Team viewer.

2.Problem solving

Code lazima zikuvuruge, ni muhimu sana kwa software developer uwe vizuri kwenye kutatua matatizo mbalimbali. Uwezo wako wa kutatua matatizo mbalimbali utakusaidia kuwa tofauti na software developer wengine.

Role zipi zinapatikana kwa software developers?

Ukijifunza software development na ukaiva utagundua kura role nyingi sana unaweza ziuza sokoni. Chini ni baadhi ya roles maarufu kwa software developer.

 1. frontend developer

Hawa ni watu wanaotengeneza website na applications, mara nyingi wanahusika kwenye muonekano wa mbele wa website na applications. Vitu vya muhimu vya kujua ili uwe front end developers mzuri ni pamoja na

Lugha basic za development ambazo ni

 • Html
 • Css
 • Javascript

Framework na Library maarufu za Css na Javascript

 • Bootstrap
 • Json
 • Xml
 • Jquery
 • Angular
 • React

Utaalamu wa kucheza na APIs

 • Rest
 • GraphQl

Data formats

 • Json
 • Xml

Tools

 • Git

2. Backend developer

Hawa ndio wale watu wanaodeal zaidi na kilicho ndani ya program zaidi kuliko ule mwonwkano wa nje ambao wengi huwa tunachanganyikiwa nao. Stadi muhimu kwa backend developer ni pamoja na

 • Backend programing language mfano python, java na php
 • Backend frameworks mfano Django, Node Js na Laravel
 • Control systems mfano AWS code commit na Gitlab
 • Database mfano My SQL, SQL, Mongo Db na PostgreSQL
 • Uelewa wa API mfano Json, SOAP na Rest.
 • Uwezo wa kuhandle server mfano Docker na Kubernets

na role nyingine zaidi

Wapi naweza jifunza software development ?

Kuna sehemu nyingi sana unazoweza jifunza software development ambapo sehemu nyingine ya kulipia na nyingine bure.Kwenye makala hii nitazungumzia fursa ya kusoma software development inayotolewa na power learn project

Power learn project ni nini?

Power learn project ni project iliyoanzishwa april 2022 na yenye lengo la kutengeneza software developer wapya milioni moja barani Afrika.Program hii kwa sasa inaendeshwa kwenye nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya, Nigeria, Zambia na Afrika kusini. Kwa sasa zaidi ya vijana 1000 wamegraduate kwenye program hii nchini kenya huku zaidi ya 7000 wakigraduate kutoka kwenye nchi zingine.

Kuna gharama yeyote ya kulipia kozi za power learn project?

Kozi ya software development kutoka power learn project ni bure kabisa endapo utapatiwa scholarship, na unaweza kutuma maombi yako ya scholarship kupitia link hii https://powerlearnproject.org/applications/Baraka

vigezo gani vinatakiwa kuomba scholarship hii?

 • Uwe na miaka zaidi ya 18
 • Uwe na laptop na internet
 • Sio lazima uwe na uzoefu wa kufanya coding

Nitapata faida zipi kuwa kwenye program hii?

 • Utakutanishwa na mentors
 • utapata nafasi ya kujiongezea ujuzi
 • utapata nafasi ya kutengeneza startup yako
 • utapewa nafasi ya kuwa sehemu ya jumuiya

Omba scholarship yako hapa https://powerlearnproject.org/applications/Baraka , hakikisha unamtumia link hii mtu unaetamani afahamu kuhusu fursa hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *