Home

Njia za kupokea malipo ya mtandaoni Tanzania

Njia za kupokea malipo ya mtandaoni Tanzania

Freelancing na kazi za mtandaoni zinakuwa kwa kasi sana nchini Tanzania na Afrika mashariki.Client kutoka nchi za Ulaya pamoja na marekani wamekuwa wakivutiwa kuajiri wafanyakazi kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.

Moja ya njia zinazotumiwa na waajiri hawa ni pamoja na kuajiri moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii kama vile Linkedin na X pamoja na kutumia majukwaa ya wauza ujuzi kama vile Upwork, Contra, Fiverr na Guru.

Mbali na uwepo wa wateja wengi wanaovutiwa na wauza ujuzi mtandaoni lakini bado suala la kupokea malipo kwenye nchi zetu bado ni changamoto.Kwenye makala hii nitazungumzia njia mbalimbali unazoweza kupokea malipo ukipata mteja wa mtandaoni.

Lakini, kabla tunzungumze kuhusu KYC ama kwa kirefu Know your customer.

KYC ni njia ambayo makampuni ya malipo yanatumia kuthibitisha taarifa za wateja kabla hawajafungua akaunti kwenye majukwaa yao.Baadhi ya hati zinazoulizwa kwenye KYC ni pamoja na

  • Kitambulisho cha uraia(NIDA)
  • Kitambulisho cha mzanzibari mkazi
  • Leseni ya udereva
  • Namba ya TIN
  • Taarifa ya benki ya kuanzia miezi mitatu
  • Kitambulisho cha mpiga kura nk

Zifuatazo ni njia zinazotumiwa na wateja wa mtandaoni kulipa wafanyakazi wao.

  1. Malipo kwenda benki za marekani.

Kampuni nyingi pamoja na wateja wengi wa ulaya wanapenda kutuma malipo kwenda kwenye akaunti za marekani kwa kutumia njia maarufu iitwayo ACH.Ukiwa Tanzania kwa sasa kuna njia tatu unazoweza kutengeneza akaunti ya benki ya marekani yenye ACH.

Njia hizo ni pamoja na Grey, Wise pamoja na Hurupay.

Hapa nitatumia Grey kama Case study

Binafsi kwa takribani miaka mitatu sasa nimekuwa nikitumia Grey kupokea malipo. Nimetumia Grey kufungua akaunti za USD, GBP na EUR.Akaunti yangu ya USD nimeiunganisha na Upwork, huku ya GBP nimeiunganisha na Etsy ile ya EUR nikipata wateja wa Ulaya huwa nawapa hiyo naitumia.

Hapa nashauri mtumie Grey kwa sababu hizi

  • Kufungua akaunti Grey ni chini ya dakika 5
  • Grey huduma yao kwa wateja iko haraka, inshort wako vizuri
  • Grey wanaruhusu kutoa hela kwa Crypto pia, ambapo mostly Crypto wanakuwaga na rate nzuri.
  • Huwa natumia kadi ya Grey kulipia vitu vya mtandaoni pia

Ukifungua akaunti Grey unaweza tumia referall code yangu: Y27RDO

Jifunze zaidi: Here’s how to get paid on Upwork in Nigeria, Kenya & Tanzania

  1. kulipwa kwa njia ya Wire.

Njia hii sishauri sana kutumiwa na watu kwani makato yake huwaga makubwa sana na pia kwa rate ambazo wanakupangia wao ambao mara nyingi huwa nzuri.Makato kwenye njia hii huanzia $20 hadi $ 50 na huchukua hadi siku 7 malipo kukufikia mahali ulipo. Kwa njia ya wire hela yako inatumwa moja kwa moja kwenda kwenye akaunti yako ya benki ya nchi uliyopo.

Kibongo bongo namaanisha unaweza kutumia akaunti za benki kama vile NMB, CRDB na Selcom kupokea malipo yako.Njia hii hutakiwi kujisajili na app yeyote bali ni benki yako ya nyumbani uliyonayo ndio hiyo hiyo unatumia kupokea.

Kupitia njia hii unaweza ulizwa kitu kinaitwa Swift code. Swift code unaweza ipata kwa kupitia website hii https://wise.com/gb/swift-codes/countries/tanzania

  1. Kulipwa kwa Payoneer na Paypal

Payoneer na Paypal ni njia ambazo pia zinapendwa na wateja pamoja na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni.Kwa Tanzania Paypal inasumbua kufungua kwani unaweza itumia kulipia tu na huwezi kutumia kupokelea malipo.

Payoneer pia inasumbua na huwa sishauri watu waitumie isipokuwa inapokuwa inapokuwa njia pekee ya kutumia. Changamoto kubwa ya payoneer ni makato makubwa unapofanya miamala na huwezi kutoa chini ya $50 na pia huwa wanatoza ada ya kila mwaka.

Kuna njia ambayo unaweza kutumia kukwepa makato makubwa kutoka Payoneer. Njia hiyo ni kwa kuunganisha akaunti yako ya Payoneer na akaunti yako ya Grey ya aidha USD, EUR ama GBP.

Pia kuna njia za panya za kuunganisha PayPal ukiwa Tanzania though sishauri hii maana PayPal wana tabia ya kufungia akaunti na wasikulipe hela zako.

Jifunze zaidi: How to withdraw Payoneer funds to a UK, EUR, or US bank account.

4.Kulipwa kwa njia ya Cryptocurrency

Hii ni moja ya njia ambayo ninaipenda na njia ya haraka zaidi yenye makato madogo. Wateja wanaotoka kwenye nchi zenye vikwazo kama vile Urusi na China wanapendelea kutumia njia hii kuwalipa wauza ujuzi.

Cryptocurrency huwa ina sarafu nyingi sana za kupokelea malipo, ila ukiwa mpya kwenye Cryptocurrency nakushauri ufungue akaunti za stablecoin kama vile USDT na USDC. USDT na USDC huwa zina value sawa na USD hivyo ni ngumu sana kuporomoka kwa haraka.

Ukiwa Tanzania nakushauri utumie Binance kufungua waleti yako ya USDT ama USDC.

Kwenye malipo ya cryptocurrency jitahidi kuwa makini kwani matapeli pia wako wengi huku.

Hizo ni njia common kwa watu wanaofanya kazi mtandaoni.Huwa ninashare madini haya kupitia group(community) yangu ya kulipia, Youtube yangu, Podcast na hata kwa kubook call na mimi Link ya huduma zangu inapatikana hapa liinks.co/mafolebarakatz

Latest Posts
Njia za kupokea malipo ya mtandaoni Tanzania
Categories
Tags
Social Media